mhanila

mhanila
KUMBUKA KAMA UNAONA PESA INAINGIA MIFUKONI UJUE IPO SIKU ITATAFUTA PAKUTOKEA

Saturday, June 30, 2012

QUOTE OF ADVICE FROM GOODBOY

TRUE LOVE isn’t about always being together. It’s about loving each other even more each day, no matter how much time you spend apart. Long distance relationship is not as difficult as many people think it is, as long as you both put in effort into your relationship. You may feel lonely & skin hungry, but once you see each other again, with every touch, hug, and kiss, it’s as if you fall in love all over again. In the end it’s all WORTH the wait. :)
@am goodboy

SIFA KUMI ZA MPENZI WA KWELI



Mpenzi msomaji wangu, ni wakati mwingine ambao tunakutana katika uwanja huu wa maisha na mapenzi, kwa lengo la kujifunza namna ya kuwa wapenzi bora na kuepukana na tatizo la kuachana ambako kumekuwa fasheni siku hizi.
Vijana wengi ambao wanapendana leo mapenzi yao hayadumu kiasi cha kubatishwa jina la utamu wa bazoka. Lakini yote hii inatokana na ukweli kwamba elimu ya mapenzi ambayo ni muhimu kwa binadamu haitolewi ipasavyo.
Ipo zana potofu kwamba kumfundisha motto mapenzi ni kumharibu, jambo ambalo si kweli bali inategemea mtoto huyo anafundishwa nini na kwa wakati gani. Lakini cha kushangaza zaidi hata watu wazima ambao ni wadau wa mapenzi hawayajui, matokeo yake wanajiingiza kwenye uhusiano wakiwa bumbumbu na hivyo kuteshwa na changamoto za mepenzi.
Leo tutajifunza kwa undani sifa kumi za mpenzi bora ili tuweze kuwatambua wapenzi wetu kabla ya kuwapa mioyo na utu wetu. Sifa hizo hizi zifuatazo.

KWANZA: Mpenzi wa kweli ni yule ambaye hatangoja kujua nini unahitaji yaani hana sababu ya kusubiri kuombwa ndiyo atoe msaada.

PILI: Ni yule atakayejua wakati gani huna furaha au una furaha na atakuwa na wewe kwa hali zote mbili .

TATU: Ni yule atayekuwa tayari kukusikiliza kwa kile utakachosema, hatojali umeongea baya au zuri .

NNE: Atakuwa na wewe wakati wa shida na raha. Hatakuacha mtu wa kuvizia vizia na kujisogeza wakati ukiwa na raha.

TANO: Mpenzi wa kweli atakuheshimu na hatopenda kuwa nyuma na kukuacha bila msaada .

SITA: Atakupenda kwa moyo wake wote na wala si kwa ajili ya shinikizo fulani (pesa au mali)

SABA: Mpenzi wa kweli ni yule atakayeonyesha kuthamini nafasi yako kama rafiki au mpenzi mbele ya wengine

NANE: Kwenye ukweli mpenzi mzuri atasema bila kukuficha na atapenda kukuonyesha mifano ya namna ya kuwa mkweli na mwaminifu.

TISA: Mpenzi wa kweli ni yule anayejiamini, asiyeyumba katika maamuzi hata kama atalazimika kufanya maamuzi magumu .

KUMI: Atakuwa tayari kuvumilia, hatakuwa mwepesi wa hasira wala kutumia lugha chafu na ubabe.
@am goodboy

ZIFAHAMU SIRI MIYONI MWA WANAWAKE.


Mwanamke anapenda kupendwa! Mara nyingi wanawake ndiyo hasa huwa na mapenzi ya dhati zaidi kuliko wanaume. Mwanamke anapoamua kuwa na mpenzi wake, humpenda kwa moyo wake wote, hivyo hupenda kuwa salama katika penzi la dhati kwako.

Anapenda uhuru, anapenda kujisikia wazi kwako mahali popote. Mwanamke anajisikia vibaya sana anapokuwa hana uhuru hata wa kukushika mkono mnakuwa barabarani pamoja. Anapenda penzi la uwazi!

Maana mwingine utakuta akikutana na rafiki yake, badala ya kumtambulisha vizuri kama mpenzi wake, anaanza kupatwa na kigugumizi. Utamsikia akisema: “Ah! Huyu ni rafiki yangu bwana, anaitwa Latipha....” hili ni kosa kubwa linalofanywa na wanaume wengi bila kujua ni kosa.

Mwanamke anakosa amani ya moyo kutokana na unavyomtafsirisha mbele ya rafiki zako. Anahisi hayupo salama. Lazima atajiuliza maswali, kwanini hataki kunitambulisha? Kwanini anashindwa kusema mimi ni mpenzi wake? Sifananii? Sina mvuto au nina tatizo gani?

Hayo yanaweza kuwa maswali yatakayomuumiza sana kichwa mpenzi wako, ambaye si ajabu akafanya maamuzi ambayo hutayapenda. Kidonda hiki hubaki moyoni mwa mwanamke, huwa vigumu sana kuonyesha wazi kwamba amechukia kutokana na uliyomfanyia, lakini atabaki akiugulia moyoni mwake kwa uchungu.

Hata hivyo, kinachokuja akilini mwake ni kutafuta mwanaume mwingine ambaye atakuwa wazi kwake ili aweze kufurahia mapenzi badala ya kuendelea kuumia moyoni mwake. Ni dhahiri kwamba uamuzi huu hautaufurahia hakika.

UNAVYOJALI...

Mwanamke anapenda awe wa pekee kwako, umsikilize, umjali na umpe kipaumbele katika kila unachokifanya . Wanawake wengi wanapenda kudekezwa, lakini hawapendi kuweka hilo wazi kwa mwanaume wake. Kwa kumtazama tu utagundua mpenzi wako anahitaji nini zaidi kwako!

Wakati mwingine anaweza kukupa mitihani ili kupima kiwango cha penzi lako. Anaweza kukuambia anaumwa au anauguliwa na mtu wake wa karibu, lengo ni kuangalia ni jinsi gani unakuwa makini anapokuwa na matatizo. Vile utakavyochukulia tatizo lake kwa ukaribu, uchungu na kuona kama lako, ndivyo utakavyomfanya aone thamani la penzi lako kwake, ikiwa vinginevyo basi humuacha na machungu moyoni, huku akijutia kuwa na mpenzi wa aina yako.

Hii ni siri ambayo si rahisi mwanamke wako akueleze moja kwa moja. Atatumia lugha ya ishara kuonesha jinsi ambavyo anahitaji kuwa wa pekee kwako.

JIFUNZE SIRI HIZO.....

Hapa ndipo mwanaume mwerevu anatakiwa kuwa makini, ni lazima ufahamu siri zilizopo moyoni mwa mpenzi wako. Jifunze kusoma hisia za mpenzi wako kwa nje, kabla ya kufanya kitu, fikiria mara mbili, lakini baada ya kufanya, msome kupitia uso wake.

Analifurahia au umemchukiza? Ni vizuri kugundua hilo ili uweze kufunga hisia za kumfanya aanze kufikiria kukusaliti. Hata mnapokuwa faragha ni vizuri kuwa makini na kila unachokifanya! Chunguza kama anafurahia penzi lako na manjonjo yote unayomfanyia.

Kumbuka kwamba ni vigumu sana mwanamke kukueleza moja kwa moja kwamba hujamfurahisha au kuna kitu umekikosea, hii husababishwa na hofu ya kuogopa kukufanya ujisikie vibaya.

Kwa maneno mengi WEWE mwanaume ndiye mwenye kazi ya kuangalia mwanamke wako anapenda nini na nini hapendi ili uweze kuwa MWANAUME wake bora, maana hata hisia zake za ndani utakuwa unazifahamu. Ni rahisi sana, soma kupitia macho yake kila unachomfanyia, utaujua ukweli. Unajua hata ukimwita kwa jina ambalo hana msisimko nalo lakini ukiwa unamtazama usoni ni rahisi sana kugundua kitu fulani, kama hajakipenda utaona kwenye macho na akikipenda pia utaona.

Unapokuwa naye faragha, tumia uwezo wako wote, lakini kumbuka kwamba si kila utakachokifanya utamfurahisha. Hii inamaanisha kwamba, baada ya kumchunguza jinsi anavyosisimka, utaweza kugundua wapi kuna msisimko zaidi kuliko sehemu nyingine.

Hapo sasa unaweza kuibuka MSHINDI maana utakuwa umeziweka siri zake hadharani, kwa maneno mengine kama yeye aliona siri, basi umeweza kuzigundua na angalau umeanza kuzifanyia kazi. Nawapenda sana rafiki zangu. Wiki ijayo nitakuja na mada nyingine mpya na nzuri zaidi.
@am goodboy

Friday, June 29, 2012

NDO SHULE HIYO TOO BADY

                                                         am out from paper hapo no ujanja
                                                          thinking of 8hrs exam daaahh
                                                  among exams done by planners student
am goodboy

Wednesday, June 27, 2012

PICTURES

JOKES

A baby boy was born in a hospital laughing instead of crying.
The more the midwives beat him the harder he laughed sundenly the doctor noticed that he had something in his hand.
So he pulled his tiny hands apart and discovered that he was holding 3 abortion pills and 5 morning after pills.
The baby looked at his mother and said.
No weapon formed against me shall prosper!
@am goodboy

3000 KUKOSA UDAHILI WA VYUO VIKUU

TUME ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), imesema kuwa wanafunzi 3000 kati ya 40,000 waliomba kujiunga na vyuo mbalimbali nchini wamekosa udahili kutokana na kasoro mbalimbali.

Katibu Mtendaji wa TCU Profesa Sifuni Mchome, aliliambia gazeti hili kuwa wanafunzi 37,000 ndio waliofanya maombi hayo kwa usahihi kupitia mfumo  unaojulikana kama  'Central Admission System', udahili wao una makosa mbalimbali.

“Jana (juzi) niliangalia na kuona wanafunzi 40,000 ndio wamefanya maombi, hao 3000 ndio wenye makosa mbalimbali, wengine wameingia tu na kufikiri ndiyo wameshafanya maombi na makosa mengine kama hayo,” alisema Profesa Mchome na kuongeza: “Barua pepe ambazo zitakuwa zimewarudia ni vyema wakazifanyia kazi kabla ya siku ya mwisho ambayo ni Juni 30.”

Alisema kuwa Julai 6 TCU itakutana na vyuo ili kupitia majina ya waombaji ambapo Julai 15 watakaa na kufanya udahili kamili kwa kuwapangia wenye sifa kwenye vyuo walivyoomba. “Nawaambia wanafunzi wasubiri huo udahili wa Julai 15,” alisema Profesa Mchome.

Katika hatua nyingine, wakuu wa vyuo na wadau wengine wa vyuo vikuu, walikutana jana jijini Dar es Salaam kujadili mfumo wa pamoja wa tuzo (University Qualification Framework). Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kujadili mfumo huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Selestine Gesimba, alisema mfumo huo utasaidia kuweka viwango sawa vya mafunzo yanayotolewa na vyuo vikuu vyote nchini.

 Katika hatua nyingine, Profesa Mchome alizungumzia wizi uliotokea katika ofisi hiyo usiku wa kuamkia juzi akisema kuwa, mali zilizopotea ni kompyuta 10 huku thamani yake ikiwa haijajulikana.
@am goodboy

SOME OF THEM

                                                    man with its mind in head
                                                                 that my identity
                                                                        am goodboy
welcome every body huku napo nko siku  mingi tufanye kazi now c unajua tena taifa nalo linatutegemea