Mwanamke anapenda kupendwa! Mara nyingi wanawake ndiyo hasa huwa na
mapenzi ya dhati zaidi kuliko wanaume. Mwanamke anapoamua kuwa na mpenzi
wake, humpenda kwa moyo wake wote, hivyo hupenda kuwa salama katika
penzi la dhati kwako.
Anapenda uhuru, anapenda kujisikia wazi
kwako mahali popote. Mwanamke anajisikia vibaya sana anapokuwa hana
uhuru hata wa kukushika mkono mnakuwa barabarani pamoja. Anapenda penzi
la uwazi!
Maana mwingine utakuta akikutana na rafiki yake,
badala ya kumtambulisha vizuri kama mpenzi wake, anaanza kupatwa na
kigugumizi. Utamsikia akisema: “Ah! Huyu ni rafiki yangu bwana, anaitwa
Latipha....” hili ni kosa kubwa linalofanywa na wanaume wengi bila kujua
ni kosa.
Mwanamke anakosa amani ya moyo kutokana na
unavyomtafsirisha mbele ya rafiki zako. Anahisi hayupo salama. Lazima
atajiuliza maswali, kwanini hataki kunitambulisha? Kwanini anashindwa
kusema mimi ni mpenzi wake? Sifananii? Sina mvuto au nina tatizo gani?
Hayo yanaweza kuwa maswali yatakayomuumiza sana kichwa mpenzi wako,
ambaye si ajabu akafanya maamuzi ambayo hutayapenda. Kidonda hiki hubaki
moyoni mwa mwanamke, huwa vigumu sana kuonyesha wazi kwamba amechukia
kutokana na uliyomfanyia, lakini atabaki akiugulia moyoni mwake kwa
uchungu.
Hata hivyo, kinachokuja akilini mwake ni kutafuta
mwanaume mwingine ambaye atakuwa wazi kwake ili aweze kufurahia mapenzi
badala ya kuendelea kuumia moyoni mwake. Ni dhahiri kwamba uamuzi huu
hautaufurahia hakika.
UNAVYOJALI...
Mwanamke anapenda
awe wa pekee kwako, umsikilize, umjali na umpe kipaumbele katika kila
unachokifanya . Wanawake wengi wanapenda kudekezwa, lakini hawapendi
kuweka hilo wazi kwa mwanaume wake. Kwa kumtazama tu utagundua mpenzi
wako anahitaji nini zaidi kwako!
Wakati mwingine anaweza kukupa
mitihani ili kupima kiwango cha penzi lako. Anaweza kukuambia anaumwa
au anauguliwa na mtu wake wa karibu, lengo ni kuangalia ni jinsi gani
unakuwa makini anapokuwa na matatizo. Vile utakavyochukulia tatizo lake
kwa ukaribu, uchungu na kuona kama lako, ndivyo utakavyomfanya aone
thamani la penzi lako kwake, ikiwa vinginevyo basi humuacha na machungu
moyoni, huku akijutia kuwa na mpenzi wa aina yako.
Hii ni siri
ambayo si rahisi mwanamke wako akueleze moja kwa moja. Atatumia lugha ya
ishara kuonesha jinsi ambavyo anahitaji kuwa wa pekee kwako.
JIFUNZE SIRI HIZO.....
Hapa ndipo mwanaume mwerevu anatakiwa kuwa makini, ni lazima ufahamu
siri zilizopo moyoni mwa mpenzi wako. Jifunze kusoma hisia za mpenzi
wako kwa nje, kabla ya kufanya kitu, fikiria mara mbili, lakini baada ya
kufanya, msome kupitia uso wake.
Analifurahia au umemchukiza?
Ni vizuri kugundua hilo ili uweze kufunga hisia za kumfanya aanze
kufikiria kukusaliti. Hata mnapokuwa faragha ni vizuri kuwa makini na
kila unachokifanya! Chunguza kama anafurahia penzi lako na manjonjo yote
unayomfanyia.
Kumbuka kwamba ni vigumu sana mwanamke kukueleza
moja kwa moja kwamba hujamfurahisha au kuna kitu umekikosea, hii
husababishwa na hofu ya kuogopa kukufanya ujisikie vibaya.
Kwa
maneno mengi WEWE mwanaume ndiye mwenye kazi ya kuangalia mwanamke wako
anapenda nini na nini hapendi ili uweze kuwa MWANAUME wake bora, maana
hata hisia zake za ndani utakuwa unazifahamu. Ni rahisi sana, soma
kupitia macho yake kila unachomfanyia, utaujua ukweli. Unajua hata
ukimwita kwa jina ambalo hana msisimko nalo lakini ukiwa unamtazama
usoni ni rahisi sana kugundua kitu fulani, kama hajakipenda utaona
kwenye macho na akikipenda pia utaona.
Unapokuwa naye faragha,
tumia uwezo wako wote, lakini kumbuka kwamba si kila utakachokifanya
utamfurahisha. Hii inamaanisha kwamba, baada ya kumchunguza jinsi
anavyosisimka, utaweza kugundua wapi kuna msisimko zaidi kuliko sehemu
nyingine.
Hapo sasa unaweza kuibuka MSHINDI maana utakuwa
umeziweka siri zake hadharani, kwa maneno mengine kama yeye aliona siri,
basi umeweza kuzigundua na angalau umeanza kuzifanyia kazi. Nawapenda
sana rafiki zangu. Wiki ijayo nitakuja na mada nyingine mpya na nzuri
zaidi.
@am goodboy
No comments:
Post a Comment