TUME ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), imesema kuwa wanafunzi 3000 kati ya
40,000 waliomba kujiunga na vyuo mbalimbali nchini wamekosa udahili
kutokana na kasoro mbalimbali.
Katibu Mtendaji wa TCU Profesa
Sifuni Mchome, aliliambia gazeti hili kuwa wanafunzi 37,000 ndio
waliofanya maombi hayo kwa usahihi kupitia mfumo unaojulikana kama
'Central Admission System', udahili wao una makosa mbalimbali.
“Jana
(juzi) niliangalia na kuona wanafunzi 40,000 ndio wamefanya maombi, hao
3000 ndio wenye makosa mbalimbali, wengine wameingia tu na kufikiri
ndiyo wameshafanya maombi na makosa mengine kama hayo,” alisema Profesa
Mchome na kuongeza: “Barua pepe ambazo zitakuwa zimewarudia ni vyema
wakazifanyia kazi kabla ya siku ya mwisho ambayo ni Juni 30.”
Alisema
kuwa Julai 6 TCU itakutana na vyuo ili kupitia majina ya waombaji
ambapo Julai 15 watakaa na kufanya udahili kamili kwa kuwapangia wenye
sifa kwenye vyuo walivyoomba. “Nawaambia wanafunzi wasubiri huo udahili
wa Julai 15,” alisema Profesa Mchome.
Katika hatua nyingine,
wakuu wa vyuo na wadau wengine wa vyuo vikuu, walikutana jana jijini Dar
es Salaam kujadili mfumo wa pamoja wa tuzo (University Qualification
Framework). Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kujadili mfumo
huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Selestine Gesimba, alisema
mfumo huo utasaidia kuweka viwango sawa vya mafunzo yanayotolewa na vyuo
vikuu vyote nchini.
Katika hatua nyingine, Profesa Mchome
alizungumzia wizi uliotokea katika ofisi hiyo usiku wa kuamkia juzi
akisema kuwa, mali zilizopotea ni kompyuta 10 huku thamani yake ikiwa
haijajulikana.
@am goodboy
No comments:
Post a Comment