mhanila

mhanila
KUMBUKA KAMA UNAONA PESA INAINGIA MIFUKONI UJUE IPO SIKU ITATAFUTA PAKUTOKEA

Monday, September 10, 2012

Ngao ya jamii Simba, Azam FC ni mechi ya kisasi kesho

KESHO Uwanja wa Taifa ‘utawaka moto’ katika pambano la kukata na shoka kati ya Simba na Azam.

Timu hizo zitapambana katika mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii ukiwa ni ufunguzi wa Ligi Kuu ya Bara, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 15.

Mechi hiyo inatarajiwa kuwa ya kisasi kwa timu hizo mbili kutokana na upinzani uliopo zinapokutana katika michuano mbalimbali.

Mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana ilikuwa ni katika michuano ya BancABC Sup8r ambapo Simba B iliifunga Azam mabao 2-0.

Azam nayo iliweka rekodi kubwa katika michuano ya Afrika Mashariki na Kati au Kombe la Kagame, kwa kuifunga Simba mabao 3-0, yote yakifungwa na John Bocco, kwenye hatua ya nusu fainali.
Simba itashuka uwanjani ikiwa na wachezaji wake wapya, baadhi ambao ni Mrisho Ngassa,
@ am goodboy

No comments:

Post a Comment