Nyie wapenzi wa soka hasa ligi ya primia mshaona hili.
Mchezaji tuseme wa Man U akicheza vizuri
uwanjani utaona mchezaji mwenzake au hata kocha wake kama Sir Alex
Furgeerson , akimpiga piga makalio...mimi nadhani ni ishara ya
pongezi..well done..well done.
Lakini Afghanistani! Weeeee. Mwiko.
Wanajeshi wa marekani au uingereza wanaohudumu
huko wamewahi kipigwa risasi kwa kuwapapasa au kumpiga piga tako
mwanajeshi wa Afghanistan.
Sasa wizara ya ulinzi ya Afghan imeamua kutoa
mafunzo maalum kwa wanajeshi wake kwamba kubalini kupapaswa makalio na
wamarekani hizo kwao ni ishara za pongezi au salamu.
Mafunzo haya maalum yanenza baada ya visa vya wanajeshi wa Afghan kuwauwa wanajeshi wa marekani katika siku za hivi karibuni.
Msemaji wa Wizari ya Ulinzi wa Afghanistan Zahir
Azimi amesema wanajeshi wote karibu laki mbili watapewa mafunzo ya
kuwaelewa Wamarekani na kukubali salamu zao.
Mwaka huu peke yake wanajeshi wa Afghan
wamewapiga risasi na kuwauwa walimu wao wa kimarekani 45. Kwa kumbe
sababu ni hizo za kupigwa pigwa makalio eti ni pongezi.
Kwa Mafghanistan hakuna pongezi za hivyo.
am goodboy
No comments:
Post a Comment