mhanila

mhanila
KUMBUKA KAMA UNAONA PESA INAINGIA MIFUKONI UJUE IPO SIKU ITATAFUTA PAKUTOKEA

Saturday, July 28, 2012

Mambo yanayokwamisha mafaniko ya kimasomo

UMASKINI
Umaskini ni kikwazo kikubwa cha mafanikio ya wanafunzi kimasomo, lakini tunashauri kwamba kila mwanafunzi anayetoka katika familia maskini ajitambue na awe tayari kuishi sawa na kipato cha familia yake wakati akitafuta elimu.
Ni muhimu kwake kubana matumizi na asiwe mtu wa kujihukumu kwa kukosa hili na lile, awe mvumilivu na mwenye kuomba msaada kila sehemu anayoona hawezi kuivuka kwa nguvu zake. Uaminifu, bidii na utii unaweza kumsaidia kuvuka kikwazo hiki.
Kuhusu suala ya kufukuzwa shule kwa kukosa ada ni vema kwa mwanafunzi mwenye kipato kidogo akawasiliana na mwalimu wake au viongozi wa serikali ili wamsaidie kutatua tatizo. Haifai kujifungia chumbani na kuanza kulia au kuamua kuacha shule kwa kukosa mahitaji. Mambo yote yanawezekana kinachotakiwa ni nia, mipango na uvumilivu.
MAPENZI
Kama kuna mtu hafahamu nini maana ya mapenzi basi kuanzia leo ajue kuwa mapenzi ni ulevi kama vilevi vingine. Mtu anayependa hulewa na kujikuta anaharibu ufahamu wake kama mtu aliyelewa pombe.
Walevi wa mapenzi huweza kufanya mapenzi hata barabarani sehemu ya wazi, huku akili zao zikiwapa taarifa kwamba watu hawawaoni, mambo ya aina hii hufanywa pia na walevi wa pombe.
Lakini ulevi wa mapenzi una nguvu kubwa ya kuiteka akili na kumtia mtu mshawasha kiasi cha kuacha kazi muhimu na kukimbilia kufanya ngono.
Hivyo, mwanafunzi ambaye anataka mafanikio ya kimasomo lazima aweke kando masuala ya mapenzi kwa lengo la kutoitwika akili mzigo ambao kwa umri wa wanafunzi wengi hasa wa kike ambao ni waitikiaji wa kauli za wavulana ni vigumu kwao kuhimili.
Licha ya baadhi ya wataalamu wa masuala ya afya kubainisha faida za kufanya mapenzi kwa afya ya mwili, bado uchunguzi unaonyesha kuwa wanafunzi wengi ambao wengi wao huwa katika umri mdogo hushindwa kuzuia hisia za mapenzi na kujikuta wanakuwa watumwa wa ngono.
Mapenzi kwa mwanafunzi yana hasara za aina mbili. Kwanza, mapenzi yanapokuwa moto huteka hisia na kumfanya msomi atumie muda mwingi kuwaza juu ya mahaba na hivyo kuufanya ubongo uone kuwa mapenzi ni kitu muhimu na hivyo kujituma kuhifadhi mambo ya mapenzi kuliko masomo.
Jambo la pili ni machungu ya mapenzi hasa yanapokuwepo mafarakano, mfano kuachwa, kusalitiwa, kuudhiwa, kugombana na migogoro yote ya kimapenzi huleta msongo wa mawazo na kumfanya mwanafunzi asiweze kusoma kwa kiwango stahili. Hivyo, inashauriwa kuwa mwanafunzi asijihusishe kabisa na mapenzi.
MIGOGORO YA KIFAMILIA
Kizuizi kingine cha kufanikiwa kimasomo kwa mwanafunzi ni kuwepo katika familia zenye migogoro. Baba na mama hawaelewani, ndugu wanagombania mali na kadhalika. Lakini inashauriwa kuwa mwanafunzi anayetoka katika familia za aina hii hatakiwi kujiingiza katika misuguano ya kifamilia.
Anachotakiwa yeye ni kuwaza juu ya masomo na kutupilia mbali mawazo yote yanayochipuka kuisumbua akili kuhusu mambo makubwa ya kiukoo. Kimsingi ufahamu wa mtoto hasa wa madarasa ya chini ni mdogo, hivyo hawezi kutatua mambo ya wazazi na akijaribu atakuwa anajisumbua na kujiweka katika matatizo makubwa zaidi.am goodboy

No comments:

Post a Comment