mhanila

mhanila
KUMBUKA KAMA UNAONA PESA INAINGIA MIFUKONI UJUE IPO SIKU ITATAFUTA PAKUTOKEA

Saturday, July 28, 2012

Watu wenye tabia hii husababisha mapenzi kuwa magumu

BILA shaka msomaji umzima bukheri wa afya na unaendelea na majukumu yako kama kawaida. Leo tunaendelea na mada yetu tuliyoianza wiki kadhaa zilizopita. Tuwemo...
Mimi kama mshauri wa saikolojia ya mapenzi, sikubaliani na hitimisho la Ali Kiba kuishi singo na kumalizana leoleo, badala yake nachochea mabadiliko chanya kwa watu ambao wamemfanya mwanamuziki huyo apate sababu ya kuyaponda mapenzi ya sasa, hivyo kutaka kila mtu awe na mtazamo wa kuwa singo.
SULUHU NI NINI
Hupaswi kuishi singo, kwani athari zake zipo. Ukisema huyataki kabisa mapenzi, kuna kundi litakalokuvalisha kesi kuwa mambo yako si mazuri. Naijua vizuri jamii yetu, mwanaume anaweza kuambiwa jongoo wake hapandi mtungi, wakati ushahidi hana.
Ukisema uwe unarukiarukia watu hovyo, kama ambavyo wengine wanafanya (kumalizana leoleo tu), huko ni kupotea sana. Maradhi yamezunguka kila upande, hivyo utajikuta unatengeneza mtandao mkubwa wa ngono bila wewe mwenyewe kujijua.
Unatakiwa kutulizana halafu ushike maelekezo ambayo tunayatoa ili kuyakabili mapenzi ya sasa. Ukimuona mwenzako bado anasumbuliwa na fikra za usistaduu badala ya kuyaheshimu mapenzi, mpishe mapema kabla hajakuumiza ukalia. Yule anayezuzuliwa na ubrazameni, mpe njia yake aende. Maisha yako ni matamu bila yeye. Zingatia.
Hatua muhimu zinaanza na wewe. Kama tabia mbaya ambazo nimekuwa nikizizungumza zipo ndani yako, tafadhali, jirekebishe haraka. Endapo wewe upo sawa na umebaini kuwa huyo unayemwita mwenzi wa maisha yako ana vitabia visivyofaa, muepuke haraka.
Ninaposema hatua muhimu zinaanza na wewe namaanisha katika pande kuu mbili. Mosi ndiyo hiyo ya wewe mwenyewe kujirekebisha pale unapoona unachemka. Pili ni kuachana na mwenzi ambaye anasumbuliwa na vitabia ambavyo nimevibainisha kinagaubaga tangu mwanzo wa makala haya.
UTAMJUAJE SISTADUU/BRAZAMENI
Nimeshakupa suluhu lakini kuna uwezekano ukawa hujafunguka inavyotakiwa. Hivyo basi, nakupa dondoo kadhaa ambazo nazichambua kwa kifupi ili kukuwezesha kutambua maana halisi ya kile ambacho nimekuwa nikikitambulisha tangu mwanzo mpaka kufikia hapa tunapokwenda kwenye tamati ya mada hii.
MTEGO WA FEDHA
Ipo wazi kuwa walengwa ni watu wanaobudu sana fedha kuliko utu. Unaweza kufanya kila linalohitajika kufanywa na wa jinsia yako kwa mpenzi wako lakini mwisho ukaishia kuumia. Utaonesha upendo na namna unavyojali lakini matokeo ya mwisho utaachwa solemba, huku ukilia kilio cha kusaga meno.
Anaweza kuwa nawe kwa sababu anavuta muda au anasubiri mambo yake yamnyookee akuache solemba.
@am goodboy

No comments:

Post a Comment